1Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya?Kwa nini unajivuna mchana kutwa,
wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?
2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.
3Unapenda mabaya kuliko mema,uongo kuliko kusema kweli.
4Unapenda kila neno lenye kudhuru,ewe ulimi wenye hila!
5Hakika Mungu atakushusha chinikwa maangamizi ya milele:atakunyakua na kukuondoa kwa nguvukutoka hema yako,
atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.
6Wenye haki wataona na kuogopa,watamcheka, wakisema,
7“Huyu ni yule mtu ambayehakumfanya Mungu kuwa ngome yake,bali alitumainia wingi wa utajiri wake,na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”
8Lakini mimi ni kama mti wa mzeituniunaostawi katika nyumba ya Mungu,nautegemea upendo wa Mungu usiokomamilele na milele.
9Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.
Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.