1Ee Mungu, sikiliza maombi yangu,wala usidharau hoja yangu.
2Nisikie na unijibu.
Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
3kwa sauti ya adui,kwa kukaziwa macho na waovu,kwa sababu wananiletea mateso juu yanguna kunitukana kwa hasira zao.
4Moyo wangu umejaa uchungu,hofu ya kifo imenishambulia.
5Woga na kutetemeka vimenizunguka,hofu kuu imenigharikisha.
6Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!Ningeruka niende mbali kupumzika.
7Ningalitorokea mbali sanana kukaa jangwani,
8ningaliharakisha kwenda mahali pa salama,mbali na tufani kali na dhoruba.”
9Ee Bwana, uwatahayarishe waovuna uwachanganyishie semi zao,
maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.
10Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake,uovu na dhuluma vimo ndani yake.
11Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini,vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.
12Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,
ningejificha asinione.
13Kumbe ni wewe, mwenzangu,mshiriki na rafiki yangu wa karibu,
14ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.
15Kifo na kiwajie adui zangu ghafula,na washuke kuzimu wangali hai,
kwa maana uovu upo ndani yao.
16Lakini ninamwita Mungu,naye Bwana huniokoa.
17Jioni, asubuhi na adhuhurininalia kwa huzuni,
naye husikia sauti yangu.
18Huniokoa nikawa salama katika vitavilivyopangwa dhidi yangu,
ingawa watu wengi hunipinga.
19Mungu anayemiliki milele,atawasikia na kuwaadhibu,watu ambao hawabadilishi njia zao,wala hawana hofu ya Mungu.
20Mwenzangu hushambulia rafiki zake,naye huvunja agano lake.
21Mazungumzo yake ni laini kama siagi,hata hivyo vita vimo moyoni mwake.Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
22Mtwike Bwana fadhaa zako,naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
23Lakini wewe, Ee Mungu,utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,hawataishi nusu ya siku zao.
Lakini mimi ninakutumaini wewe.