Inapakia...
šŸ“–

Biblia Takatifu

BiblicaĀ® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifuā„¢
BIB • 11 mistari

Zaburi 58

Zaburi • Sura 58 / 150

Mungu Kuwaadhibu Waovu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa ā€œUsiharibu!ā€ Utenzi wa Daudi.

1Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki?Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu?

2La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu,na mikono yenu hupima jeuri duniani.

3Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,toka tumboni mwa mama zao
ni wakaidi na husema uongo.

4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka,kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

5ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi,hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani.

6Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao;Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba!

7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi,wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu.

8Kama konokono ayeyukavyo akitembea,kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu,
wasilione jua.

9Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba,zikiwa mbichi au kavu,waovu watakuwawamefagiliwa mbali.

10Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi,watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu.

11Ndipo wanadamu watasema,ā€œHakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu,
hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.ā€