Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 10 mistari

Zaburi 6

Zaburi • Sura 6 / 150

Sala Kwa Ajili Ya Msaada Wakati Wa Taabu
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.*Zaburi ya Daudi.

1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.

2Unirehemu Bwana,kwa maana nimedhoofika;Ee Bwana, uniponye,kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.

3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini?

4Geuka Ee Bwana, unikomboe,uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.

5Hakuna mtu anayekukumbukaakiwa amekufa.Ni nani awezaye kukusifuakiwa kuzimu?

6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;usiku kucha nafurikisha
kitanda changu kwa machozi;nimelowesha viti vyangu vya faharikwa machozi.

7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.

8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu.

9Bwana amesikia kilio changu kwa huruma,Bwana amekubali sala yangu.

10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.

Tanbihi

*

Sheminithi ni mtajo mmojawapo katika lugha ya uimbaji.