Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 8 mistari

Zaburi 61

Zaburi • Sura 61 / 150

Kuomba Ulinzi
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za uimbaji. Zaburi ya Daudi.

1Ee Mungu, sikia kilio changu,usikilize maombi yangu.

2Kutoka miisho ya dunia ninakuita,ninaita huku moyo wangu unadhoofika;uniongoze kwenye mwambaule ulio juu kuliko mimi.

3Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu,ngome imara dhidi ya adui.

4Natamani kukaa hemani mwako milele,na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

5Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu,umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

6Mwongezee mfalme siku za maisha yake,miaka yake kwa vizazi vingi.

7Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele;amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

8Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lakona kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.