Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,waaibishwe na kufadhaishwa;wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4Lakini wote wakutafutaowashangilie na kukufurahia,wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,“Mungu na atukuzwe!”
5Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;Ee Mungu, unijie haraka.Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;Ee Bwana, usikawie.