Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 20 mistari

Zaburi 72

Zaburi • Sura 72 / 150

Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme
Zaburi ya Solomoni.

1Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,mwana wa mfalme kwa haki yako.

2Atawaamua watu wako kwa haki,watu wako walioonewa kwa haki.

3Milima italeta mafanikio kwa watu,vilima tunda la haki.

4Atawatetea walioonewa miongoni mwa watuna atawaokoa watoto wa wahitaji,
ataponda mdhalimu.

5Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.

6Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,kama manyunyu yanyeshayo ardhi.

7Katika siku zake wenye haki watastawi;mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.

8Atatawala kutoka bahari hadi baharina kutoka Mto*mpaka miisho ya dunia.

9Makabila ya jangwani watamsujudia,na adui zake wataramba mavumbi.

10Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbaliwatamletea kodi;wafalme wa Sheba na Sebawatampa zawadi.

11Wafalme wote watamsujudiana mataifa yote yatamtumikia.

12Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.

13Atawahurumia wanyonge na wahitajina kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.

14Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.

15Aishi maisha marefu!Na apewe dhahabu ya Sheba.Watu wamwombee daimana kumbariki mchana kutwa.

16Nafaka ijae tele katika nchi yote,juu ya vilele vya vilima na istawi.Tunda lake na listawi kama Lebanoni,listawi kama majani ya kondeni.

17Jina lake na lidumu milele,na lidumu kama jua.
Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,nao watamwita aliyebarikiwa.

18Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.

19Jina lake tukufu lisifiwe milele,ulimwengu wote ujae utukufu wake.Amen na Amen.

20Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.

Tanbihi

*

Yaani Mto Frati.