1Ee Mungu, tunakushukuru,tunakushukuru wewe,kwa kuwa jina lako li karibu;watu husimulia matendo yako ya ajabu.
2Unasema, “Ninachagua wakati maalum;ni mimi nihukumuye kwa haki.
3Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.
4Kwa wale wenye majivuno ninasema,‘Msijisifu tena,’
kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.
5Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”
6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibiau kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.
7Bali Mungu ndiye ahukumuye:Humshusha huyu na kumkweza mwingine.
8Mkononi mwa Bwana kuna kikombekilichojaa mvinyo unaotoka povu
uliochanganywa na vikolezo;huumimina, nao waovu wote wa duniahunywa mpaka tone la mwisho.
9Bali mimi, nitatangaza hili milele;nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.
10Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.