Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 7 mistari

Zaburi 87

Zaburi • Sura 87 / 150

Sifa Za Yerusalemu
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;

2Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.

3Mambo matukufu yanasemwa juu yako,ee mji wa Mungu:

4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu*na Babelimiongoni mwa wale wanaonikubali mimi:Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,*nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,“Huyu na yule walizaliwa humo,naye Aliye Juu Sana mwenyeweatamwimarisha.”

6Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:“Huyu alizaliwa Sayuni.”

7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”

Tanbihi

*

Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.

*

Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.