Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 9 mistari

Zaburi 99

Zaburi • Sura 99 / 150

Mungu Mfalme Mkuu

1Bwana anatawala,mataifa na yatetemeke;anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,dunia na itikisike.

2Bwana ni mkuu katika Sayuni;ametukuzwa juu ya mataifa yote.

3Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:yeye ni mtakatifu!

4Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,wewe umethibitisha adili;katika Yakobo umefanyayaliyo haki na sawa.

5Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;
yeye ni mtakatifu.

6Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;walimwita Bwana,naye aliwajibu.

7Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;walizishika sheria zake na amri alizowapa.

8Ee Bwana, wetu,ndiwe uliyewajibu,kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9Mtukuzeni Bwana Mungu wetu,mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,
kwa maana Bwana Mungu wetu ni mtakatifu.