1Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote.
2Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka mawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema,
3âMsiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.â
4Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka makabila yote ya Israeli.
5Kutoka kabila la Yuda 12,000 walitiwa muhuri, kutoka kabila la Reubeni 12,000, kutoka kabila la Gadi 12,000,
6kutoka kabila la Asheri 12,000, kutoka kabila la Naftali 12,000, kutoka kabila la Manase 12,000,
7kutoka kabila la Simeoni 12,000, kutoka kabila la Lawi 12,000, kutoka kabila la Isakari 12,000,
8kutoka kabila la Zabuloni 12,000, kutoka kabila la Yosefu 12,000, na kutoka kabila la Benyamini 12,000.
9Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.
10Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema:âWokovu una Mungu wetu,yeye aketiye kwenye kiti cha enzi,
na Mwana-Kondoo!â
11Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu,
12wakisema:âAmen!Sifa na utukufuna hekima na shukrani na heshimana uweza na nguvuviwe kwa Mungu wetu milele na milele.Amen!â
13Kisha mmoja wa wale wazee ishirini na wanne akaniuliza, âNi nani hawa waliovaa mavazi meupe, nao wametoka wapi?â
14Nikamjibu, âBwana, wewe wajua.â Naye akasema, âHawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa.
15Kwa hiyo,âWako mbele ya kiti cha enzi cha Munguna kumtumikia usiku na mchana
katika hekalu lake;naye aketiye katika kile kiti cha enziatatanda hema yake juu yao.
16Kamwe hawataona njaawala kiu tena.Jua halitawapigawala joto lolote liunguzalo.
17Kwa maana Mwana-Kondooaliyeko katikati ya kile kiti cha enzi
atakuwa Mchungaji wao;naye atawaongoza kwendakwenye chemchemi za maji yaliyo hai.Naye Mungu atafuta kila chozikutoka macho yao.â