1Laiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa kiume,ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu!Kisha, kama ningekukuta huko nje,ningelikubusu,
wala hakuna mtu yeyote angelinidharau.
2Ningelikuongoza na kukuletakatika nyumba ya mama yangu,
yeye ambaye amenifundisha.Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe,asali ya maua ya mikomamanga yangu.
3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu,na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
4Binti za Yerusalemu, ninawaagiza:msichochee wala kuamsha mapenzi
hata yatakapotaka yenyewe.
5Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikaniakimwegemea mpenzi wake?MpendwaNilikuamsha chini ya mtofaa,huko mama yako alipotunga mimba yako,
huko yeye alipata utungu akakuzaa.
6Nitie kama muhuri moyoni mwako,kama muhuri kwenye mkono wako;kwa maana upendo una nguvu kama mauti,wivu wake ni mkatili kama kuzimu.Unachoma kama mwali wa moto,kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa.
7Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,mito haiwezi kuugharikisha.Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwakekwa ajili ya upendo,
angelidharauliwa kabisa.
8Tunaye dada mdogo,matiti yake hayajakua bado.Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetuwakati atakapokuja kuposwa?
9Kama yeye ni ukuta,tutajenga minara ya fedha juu yake.Na kama yeye ni mlango,tutamzungushia mbao za mierezi.
10Mimi ni ukuta,nayo matiti yangu ni kama minara.Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pakekama yule anayeleta utoshelevu.
11Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni;alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji.Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yakeshekeli 1,000*za fedha.
12Lakini shamba langu la mizabibuambalo ni langu mwenyewe
ni langu kutoa;hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni,na shekeli mia mbili*ni kwa ajili
ya wale wanaotunza matunda yake.
13Wewe ukaaye bustaninipamoja na marafiki mliohudhuria,
hebu nisikie sauti yako!
14Njoo, mpenzi wangu,uwe kama swalaau kama ayala kijanajuu ya milima iliyojaa vikolezo.
Tanbihi
Shekeli 1,000 ni kama kilo 11.5.
Shekeli 200 ni kama kilo 2.3.