1Kisha akanionyesha Yoshua,*kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
2Bwana akamwambia Shetani, âBwana akukemee Shetani! Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?â
3Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.
4Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, âMvueni hizo nguo zake chafu.â Kisha akamwambia Yoshua, âTazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.â
5Kisha nikasema, âMvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.â Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu.
6Malaika wa Bwana akamwamuru Yoshua:
7âHivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: âIkiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
8â âSikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
9Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ânami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
10â âKatika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,â asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.â
Tanbihi
Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu.