1Kusanyikeni pamoja, kusanyikeni pamoja,enyi taifa lisilo na aibu,
2kabla ya wakati ulioamriwa haujafikana siku ile inayopeperusha kama makapi,kabla hasira kali ya Bwana haijaja juu yenu,kabla siku ya ghadhabu ya Bwana
haijaja juu yenu.
3Mtafuteni Bwana, enyi nyote wanyenyekevu wa nchi,ninyi ambao hufanya lile analoamuru.Tafuteni haki, tafuteni unyenyekevu;labda mtahifadhiwa
siku ya hasira ya Bwana.
4Gaza utaachwana Ashkeloni utaachwa magofu.Wakati wa adhuhuri Ashdodi utaachwa mtupuna Ekroni utangʼolewa.
5Ole wenu ninyi ambao mnaishi kando ya bahari,enyi Wakerethi;neno la Bwana liko dhidi yenu,ee Kanaani, nchi ya Wafilisti.
“Mimi nitawaangamiza,na hakuna atakayebaki.”
6Nchi kando ya bahari, mahali ambapo wanaishi Wakerethi,patakuwa mahali pa wachungaji
na mazizi ya kondoo.
7Itakuwa mali ya mabaki ya nyumba ya Yuda,hapo watapata malisho.Wakati wa jioni watajilaza chinikatika nyumba za Ashkeloni.Bwana Mungu wao atawatunza,naye atawarudishia wafungwa wao.
8“Nimeyasikia matukano ya Moabunazo dhihaka za Waamoni,ambao waliwatukana watu wanguna kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.
9Hakika, kama niishivyo,”asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mungu wa Israeli,“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,Waamoni kama Gomora:mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,nchi ya ukiwa milele.Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”
10Hiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,kwa kutukana na kudhihaki
watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.
11Bwana atakuwa wa kuhofisha kwaoatakapoangamiza miungu yote ya nchi.Mataifa katika kila pwani yatamwabudu,kila moja katika nchi yake.
12“Ninyi pia, ee Wakushi,mtauawa kwa upanga wangu.”
13Mungu atanyoosha mkono wake dhidi ya kaskazinina kuangamiza Waashuru,akiiacha Ninawi ukiwana pakame kama jangwa.
14Makundi ya kondoo na ngʼombe yatajilaza pale,viumbe vya kila aina.Bundi wa jangwani na bundi waliao kwa sauti nyembambawataishi juu ya nguzo zake.Mwangwi wa kuita kwao utapita madirishani,kifusi kitakuwa milangoni,
boriti za mierezi zitaachwa wazi.
15Huu ndio mji uliotukuka na kuishi kwa furahawakijisikia salama.Ulisema moyoni mwako,“Mimi ndimi, na wala hapana mwingine ila mimi.”Jinsi gani umekuwa gofu,mahali pa kulala wanyama pori!Wote wanaopita kando yake wanauzomeana kutikisa mkono kwa dharau.