Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 16 mistari

Amosi 2

Amosi • Sura 2 / 9

1Hili ndilo asemalo Bwana:“Kwa dhambi tatu za Moabu,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,ikawa kama chokaa.

2Nitatuma moto juu ya Moabuambao utateketeza ngome za Keriothi.Moabu ataanguka kwa ghasia kubwakatikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta.

3Nitamwangamiza mtawala wakena kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”asema Bwana.

4Hili ndilo asemalo Bwana:“Kwa dhambi tatu za Yuda,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwanana hawakuzishika amri zake,kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,miungu ambayo babu zao waliifuata.

5Nitatuma moto juu ya Yudaambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”

Hukumu Juu Ya Israeli

6Hili ndilo asemalo Bwana:“Kwa dhambi tatu za Israeli,hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.Wanawauza wenye haki kwa fedha,na maskini kwa jozi ya viatu.

7Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,kama vile juu ya mavumbi ya nchi,
na kukataa haki kwa walioonewa.Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.

8Watu hulala kando ya kila madhabahujuu ya nguo zilizowekwa rehani.Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyoulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.

9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao,ingawa alikuwa mrefu kama mierezi,
na mwenye nguvu kama mialoni.Niliyaangamiza matunda yake juuna mizizi yake chini.

10“Niliwapandisha toka Misri,na nikawaongoza miaka arobaini jangwani
niwape nchi ya Waamori.

11Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenuna Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu.Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?”asema Bwana.

12“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyona kuwaamuru manabii wasitoe unabii.

13“Sasa basi, nitawapondakama gari lipondavyo wakati limejazwa nafaka.

14Mkimbiaji hodari hatanusurika,wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,
na shujaa hataweza kuokoa maisha yake.

15Mpiga upinde atakimbia,askari wapiga mbio hawataweza kutoroka,
na mpanda farasi hataokoa maisha yake.

16Hata askari walio mashujaa sanasiku hiyo watakimbia uchi,”asema Bwana.