Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 15 mistari

Amosi 3

Amosi • Sura 3 / 9

Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli

1Sikilizeni neno hili alilosema Bwana dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri:

2“Ni ninyi tu niliowachaguakati ya jamaa zote za dunia;kwa hiyo nitawaadhibukwa ajili ya dhambi zenu zote.”

3Je, watu wawili hutembea pamojawasipokubaliana kufanya hivyo?

4Je, simba hunguruma katika kichakawakati hana mawindo?Aweza kuvuma katika pangowakati ambao hajakamata chochote?

5Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhiniambapo hajategewa chambo?Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhiniwakati ambapo hakuna chochote cha kunasa?

6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,watu hawatetemeki?Mji upatwapo na maafa,je, si Bwana amesababisha?

7Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolotebila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

8Simba amenguruma:je, ni nani ambaye hataogopa?Bwana Mwenyezi ametamka:je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?

9Tangazeni katika ngome za Ashdodina katika ngome za Misri:“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,
na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.”

10Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,wale ambao hujilundikia nyara
na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”

11Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:“Adui ataizingira nchi;ataangusha chini ngome zenu
na kuteka nyara maboma yenu.”

12Hili ndilo asemalo Bwana:“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simbavipande viwili tu vya mfupa wa mguu
au kipande cha sikio,hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,wale wakaao Samaria
kwenye kingo za vitanda vyao,na katika Dameskikwenye viti vyao vya fahari.”

13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

14“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,nitaharibu madhabahu za Betheli;pembe za madhabahu zitakatiliwa mbalina kuanguka chini.

15Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovuna majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”asema Bwana.