Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 11 mistari

Hosea 6

Hosea • Sura 6 / 14

Israeli Asiye Na Toba

1“Njooni, tumrudie Bwana.
Ameturarua vipande vipandelakini atatuponya;ametujeruhi lakiniatatufunga majeraha yetu.

2Baada ya siku mbili atatufufua;katika siku ya tatu atatuinua,
ili tuweze kuishi mbele zake.

3Tumkubali Bwana,tukaze kumkubali yeye.Kutokea kwake ni hakika kama vilekuchomoza kwa jua;atatujia kama mvua za masika,kama vile mvua za vuli
ziinyweshavyo nchi.”

4“Nifanye nini nawe, Efraimu?Nifanye nini nawe, Yuda?Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi,kama umande wa alfajiri utowekao.

5Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipandekwa kutumia manabii wangu;nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu,hukumu zangu zinawaka
kama umeme juu yenu.

6Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu,kumkubali Mungu zaidi
kuliko sadaka za kuteketezwa.

7Wamevunja Agano kama Adamu:huko hawakuwa waaminifu kwangu.

8Gileadi ni mji wenye watu waovu,umetiwa madoa kwa nyayo za damu.

9Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu,ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo;wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu,wakifanya uhalifu wa aibu.

10Nimeona jambo la kutishakatika nyumba ya Israeli.Huko Efraimu amejitolea kwa ukahabana Israeli amenajisika.

11“Pia kwa ajili yako, Yuda,mavuno yameamriwa.
“Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu,