Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 16 mistari

Hosea 7

Hosea • Sura 7 / 14

1kila mara nilipotaka kumponya Israeli,dhambi za Efraimu zinafichuliwa
na maovu ya Samaria yanafunuliwa.Wanafanya udanganyifu,wevi huvunja nyumba,
maharamia hunyangʼanya barabarani,

2lakini hawafahamu kwambaninakumbuka matendo yao yote mabaya.Dhambi zao zimewameza,ziko mbele zangu siku zote.

3“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,wakuu wao kwa uongo wao.

4Wote ni wazinzi,wanawaka kama tanuruambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchocheakuanzia kukanda unga
hadi umekwisha kuumuka.

5Katika sikukuu ya mfalme wetuwakuu wanawaka kwa mvinyo,
naye anawaunga mkono wenye mizaha.

6Mioyo yao ni kama tanuru,wanamwendea kwa hila.Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,wakati wa asubuhi inalipuka
kama miali ya moto.

7Wote ni moto kama tanuru;wanawaangamiza watawala wao.Wafalme wake wote wanaanguka,wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.

8“Efraimu anajichanganya na mataifa;Efraimu ni mkate ambao haukuiva.

9Wageni wananyonya nguvu zake,lakini hafahamu hilo.Nywele zake zina mvi hapa na pale,lakini hana habari.

10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,lakini pamoja na haya yoteharudi kwa Bwana Mungu wakewala kumtafuta.

11“Efraimu ni kama hua,hudanganywa kwa urahisi na hana akili:mara anaita Misri,mara anageukia Ashuru.

12Wakati watakapokwenda,nitatupa wavu wangu juu yao;nitawavuta chini waangukekama ndege wa angani.Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,nitawanasa.

13Ole wao, kwa sababuwamepotoka kutoka kwangu!Maangamizi ni yaokwa sababu wameniasi!Ninatamani kuwakomboa,lakini wanasema uongo dhidi yangu.

14Hawanililii mimi kutoka mioyoni mwao,bali wanaomboleza vitandani mwao.Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya,lakini hugeukia mbali nami.

15Niliwafundisha na kuwatia nguvu,lakini wanapanga mabaya dhidi yangu.

16Hawamgeukii Yeye Aliye Juu Sana,wako kama upinde wenye kasoro.Viongozi wao wataanguka kwa upangakwa sababu ya maneno yao ya jeuri.Kwa ajili ya hili watadhihakiwakatika nchi ya Misri.