1Usifurahie, ee Israeli;usishangilie kama mataifa mengine.Kwa kuwa hukuwamwaminifu kwa Mungu wako;umependa ujira wa kahaba kwenye kila sakafuya kupuria nafaka.
2Sakafu za kupuria nafaka na mashinikizo ya kukamulia divaihavitalisha watu,
divai mpya itawapungukia.
3Hawataishi katika nchi ya Bwana,Efraimu atarudi Misrina atakula chakulakilicho najisi huko Ashuru.
4Hawatammiminia Bwana sadaka ya divaiwala dhabihu zao hazitampendeza.Dhabihu kama hizo zitakuwa kwaokama mkate wa waombolezaji;
nao wote wazilao watakuwa najisi.Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe;kisije katika Hekalu la Bwana.
5Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa,katika siku za sikukuu za Bwana?
6Hata ikiwa wataokoka maangamizi,Misri atawakusanya,
nayo Memfisi*itawazika.Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma,nayo miiba itafunika mahema yao.
7Siku za adhabu zinakuja,siku za malipo zimewadia.
Israeli na afahamu hili.Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sanana uadui wenu ni mkubwa sana,nabii anadhaniwa ni mpumbavu,mtu aliyeongozwa na Mungu
anaonekana mwendawazimu.
8Nabii, pamoja na Mungu wangu,ndiye mlinzi juu ya Efraimu,hata hivyo mitego inamngojeakatika mapito yake yote,
na uadui katika nyumba ya Mungu wake.
9Wamezama sana katika rushwa,kama katika siku za Gibea.Mungu atakumbuka uovu waona kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.
10“Nilipompata Israeli, ilikuwa kamakupata zabibu jangwani;nilipowaona baba zenu, ilikuwa kama kuonamatunda ya kwanza katika mtini.Lakini walipofika Baal-Peori, walijiweka wakfukwa ile sanamu ya aibu,nao wakawa najisikama kitu kile walichokipenda.
11Utukufu wa Efraimu utaruka kama ndege:hakuna kuzaa, hakuna kuchukua mimba,
hakuna kutunga mimba.
12Hata wakilea watoto,nitamuua kila mmoja.Ole waonitakapowapiga kisogo!
13Nimemwona Efraimu, kama Tiro,aliyeoteshwa mahali pazuri.Lakini Efraimu wataletawatoto wao kwa mchinjaji.”
14Wape, Ee Bwana,je, utawapa nini?Wape matumbo ya kuharibu mimbana matiti yaliyokauka.
15“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali,niliwachukia huko.Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi,nitawafukuza katika nyumba yangu.Sitawapenda tena,viongozi wao wote ni waasi.
16Efraimu ameharibiwa,mzizi wao umenyauka,
hawazai tunda.Hata kama watazaa watoto,nitawachinja watoto wao
waliotunzwa vizuri.”
17Mungu wangu atawakataakwa sababu hawakumtii;watakuwa watu wa kutangatangamiongoni mwa mataifa.
Tanbihi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.