1âWekeni tarumbeta midomoni mwenu!Tai yuko juu ya nyumba ya Bwanakwa sababu watu wamevunja Agano langu,wameasi dhidi ya sheria yangu.
2Israeli ananililia,âEe Mungu wetu, tunakukubali!â
3Lakini Israeli amekataa lile lililo jema,adui atamfuatia.
4Wanaweka wafalme bila idhini yangu,wamechagua wakuu bila kibali changu.Kwa fedha zao na dhahabuwamejitengenezea sanamu kwa ajili
ya maangamizi yao wenyewe.
5Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama!Hasira yangu inawaka dhidi yao.Watakuwa najisi mpaka lini?
6Zimetoka katika Israeli!Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu.Atavunjwa vipande vipande,
yule ndama wa Samaria.
7âWanapanda upepona kuvuna upepo wa kisulisuli.Bua halina suke,halitatoa unga.Kama lingetoa nafaka,wageni wangeila yote.
8Israeli amemezwa;sasa yupo miongoni mwa mataifa
kama kitu kisicho na thamani.
9Kwa kuwa wamepanda kwenda Ashurukama punda-mwitu anayetangatanga peke yake.Efraimu amejiuza mwenyewekwa wapenzi.
10Ingawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa,sasa nitawakusanya pamoja.Wataanza kudhoofika chini ya uonevuwa mfalme mwenye nguvu.
11âIngawa Efraimu alijenga madhabahu nyingikwa ajili ya sadaka za dhambi,hizi zimekuwa madhabahuza kufanyia dhambi.
12Nimeandika kwa ajili yao mambo mengikuhusu sheria yangu,lakini wameziangaliakama kitu cha kigeni.
13Wanatoa dhabihu nilizopewa miminao wanakula hiyo nyama,
lakini Bwana hapendezwi nao.Sasa ataukumbuka uovu waona kuadhibu dhambi zao:
Watarudi Misri.
14Israeli amemsahau Muumba wakena kujenga majumba ya kifalme,
Yuda amejengea miji mingi ngome.Lakini nitatuma moto kwenye miji yaoutakaoteketeza ngome zao.â