Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 16 mistari

Isaya 11

Isaya • Sura 11 / 66

Tawi Kutoka Kwa Yese

1Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese,kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.

2Roho wa Bwana atakaa juu yake,Roho wa hekima na wa ufahamu,
Roho wa shauri na wa uweza,
Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana

3naye atafurahia kumcha Bwana.
Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,

4bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.

5Haki itakuwa mkanda wakena uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.

6Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo,naye chui atalala pamoja na mbuzi,ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja,naye mtoto mdogo atawaongoza.

7Ngʼombe na dubu watalisha pamoja,watoto wao watalala pamoja,
na simba atakula majani makavu kama maksai.

8Mtoto mchanga atacheza karibu na shimo la nyoka,
naye mtoto mdogo ataweka mkono wakekwenye kiota cha fira.

9Hawatadhuru wala kuharibujuu ya mlima wangu mtakatifu wote,kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwanakama maji yajazavyo bahari.

10Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.

11Katika siku hiyo Bwana atanyoosha mkono wake mara ya pili kurudisha mabaki ya watu wake waliosalia kutoka Ashuru, Misri, Pathrosi,*Kushi, Elamu, Babeli, Hamathi na kutoka visiwa vya baharini.

12Atainua bendera kwa mataifana kuwakusanya Waisraeli walioko uhamishoni;atawakusanya watu wa Yuda waliotawanyikakutoka pembe nne za dunia.

13Wivu wa Efraimu utatoweka,na adui wa Yuda watakatiliwa mbali;Efraimu hatamwonea Yuda wivu,wala Yuda hatakuwa na uadui na Efraimu.

14Watawashukia katika miteremko ya Wafilistihadi upande wa magharibi,kwa pamoja watawateka watu nyarahadi upande wa mashariki.Watawapiga Edomu na Moabu,na Waamoni watatawaliwa nao.

15Bwana atakaushaghuba ya bahari ya Misri;kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wakejuu ya Mto Frati.Ataugawanya katika vijito sabaili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.

16Itakuwepo njia kuu kwa mabaki ya watu wakewale waliosalia kutoka Ashuru,kama ilivyokuwa kwa Israeliwalipopanda kutoka Misri.

Tanbihi

*

Pathrosi ina maana Misri ya Juu.