Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 12 mistari

Isaya 53

Isaya • Sura 53 / 66

1Ni nani aliyeamini ujumbe wetu,na mkono wa Bwana umefunuliwa kwa nani?

2Alikua mbele yake kama mche mwororona kama mzizi katika nchi kavu.Hakuwa na uzuri wala utukufu wa kutuvutia kwake,hakuwa na chochote katika sura yake cha kutufanya tumtamani.

3Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu,mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso.Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.

4Hakika alichukua udhaifu wetuna akajitwika huzuni zetu,hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu,akapigwa sana naye, na kuteswa.

5Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu,alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,na kwa majeraha yake sisi tumepona.

6Sisi sote, kama kondoo, tumepotea,kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe,naye Bwana aliweka juu yakemaovu yetu sisi sote.

7Alionewa na kuteswa,hata hivyo hakufungua kinywa chake;aliongozwa kama mwana-kondooapelekwaye machinjoni,kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya,hivyo hakufungua kinywa chake.

8Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa.Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai,alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.

9Wakamfanyia kaburi pamoja na waovu,pamoja na matajiri katika kifo chake,ingawa hakutenda jeuri,wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwanakumchubua na kumsababisha ateseke.Ingawa Bwana amefanya maisha yakekuwa sadaka ya hatia,ataona uzao wake na kuishi siku nyingi,nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.

11Baada ya maumivu ya nafsi yake,ataona nuru ya uzima na kuridhika;kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye hakiatawafanya wengi kuwa wenye haki,
naye atayachukua maovu yao.

12Kwa hiyo nitamgawia sehemu miongoni mwa wakuu,naye atagawana nyara pamoja na wenye nguvu,kwa sababu aliyamimina maisha yake hadi mauti,naye alihesabiwa pamoja na wakosaji.Kwa kuwa alichukua dhambi za wengi,na kuwaombea wakosaji.