Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 21 mistari

Isaya 57

Isaya • Sura 57 / 66

Ibada Ya Sanamu Ya Israeli Iliyo Batili

1Mwenye haki hupotea,wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake;watu wanaomcha Mungu huondolewa,wala hakuna hata mmoja anayeelewakuwa wenye haki wameondolewaili wasipatikane na maovu.

2Wale waendao kwa unyofuhuwa na amani;
hupata pumziko walalapo mautini.

3“Lakini ninyi:Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,
ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!

4Mnamdhihaki nani?Ni nani mnayemcheka kwa dharau,
na kumtolea ndimi zenu?
Je, ninyi si watoto wa waasi,
uzao wa waongo?

5Mnawaka tamaa katikati ya mialonina chini ya kila mti uliotanda matawi;mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabondena chini ya majabali yenye mianya.

6“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu;hizo ndizo sehemu yenu.Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji,na kutoa sadaka za nafaka.Katika haya yote,niendelee kuona huruma?

7Umeweka kitanda chako juu kwenye kilima kirefu kilichoinuka,huko ulikwenda kutoa dhabihu zako.

8Nyuma ya milango yako na miimo yakoumeweka alama zako za kipagani.Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako,umepanda juu yake na kukipanua sana;ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao,nawe uliangalia uchi wao.

9Ulikwenda kwa Moleki*ukiwa na mafuta ya zeituni,na ukaongeza manukato yako.Ukawatuma wajumbe wako mbali sana,ukashuka kwenye kaburi*lenyewe!

10Ulikuwa umechoshwa na njia zako zote,lakini hukusema, ‘Hakuna tumaini.’Ulipata uhuisho wa nguvu zako,kwa sababu hiyo hukuzimia.

11“Ni nani uliyemhofu hivyo na kumwogopahata ukawa mwongo kwangu,wala hukunikumbukaau kutafakari hili moyoni mwako?Si ni kwa sababu nimekuwa kimya muda mrefuhata huniogopi?

12Nitaifunua haki yako na matendo yako,nayo hayatakufaidi.

13Utakapolia kwa kuhitaji msaada,sanamu zako ulizojikusanyia na zikuokoe!Upepo utazipeperusha zote,pumzi peke yake itazipeperusha,Lakini mtu atakayenifanya kimbilio lake,atairithi nchi
na kuumiliki mlima wangu mtakatifu.”

Faraja Kwa Wenye Majuto

14Tena itasemwa:“Jengeni, jengeni, itengenezeni njia!Ondoeni vikwazo katika njia ya watu wangu.”

15Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana,yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu:“Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu,
lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubuna mwenye roho ya unyenyekevu,ili kuzihuisha roho za wanyenyekevuna kuihuisha mioyo yao waliotubu.

16Sitaendelea kulaumu milele,wala sitakasirika siku zote,kwa kuwa roho ya mwanadamuingezimia mbele zangu:
yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.

17Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi;nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira,
na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.

18Nimeziona njia zake, lakini nitamponya,nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,

19nikiumba sifa midomoni ya waombolezajikatika Israeli.Amani, amani, kwa wale walio mbalina kwa wale walio karibu,”
asema Bwana. “Nami nitawaponya.”

20Bali waovu ni kama bahari ichafukayo,ambayo haiwezi kutulia,
mawimbi yake hutupa takataka na matope.

21Mungu wangu asema,“Hakuna amani kwa waovu.”

Tanbihi

*

Moleki alikuwa mungu aliyekuwa anaabudiwa na Waamoni; pia alijulikana kama Malkomu, Maloki au Kemoshi wa Moabu.

*

Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.