Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 14 mistari

Isaya 58

Isaya • Sura 58 / 66

Mfungo Wa Kweli

1“Piga kelele, usizuie.Paza sauti yako kama tarumbeta.Watangazieni watu wangu uasi wao,na kwa nyumba ya Yakobo dhambi zao.

2Kwa maana kila siku hunitafuta,wanaonekana kutaka kujua njia zangu,kana kwamba walikuwa taifa linalotenda lililo sawa,na ambalo halijaziacha amri za Mungu wake.Hutaka kwangu maamuzi ya haki,nao hutamani Mungu awakaribie.

3Wao husema, ‘Mbona tumefunga, nawe hujaona?Mbona tumejinyenyekeza, nawe huangalii?’
“Lakini katika siku ya kufunga kwenu, mnafanya mnavyotakana kuwadhulumu wafanyakazi wenu wote.

4Kufunga kwenu huishia kwenye magomvi na mapigano,na kupigana ninyi kwa ninyi kwa ngumi za uovu.Hamwezi kufunga kama mnavyofanya leona kutazamia sauti zenu kusikiwa huko juu.

5Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua,siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza?Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete,na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu?Je, huo ndio mnaouita mfungo,siku iliyokubalika kwa Bwana?

6“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua:kufungua minyororo ya udhalimu,
na kufungua kamba za nira,kuwaweka huru walioonewa,na kuvunja kila nira?

7Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaana kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi,unapomwona aliye uchi, umvike,wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?

8Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazukona uponyaji wako utatokea upesi;ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako,na utukufu wa Bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.

9Ndipo utaita, naye Bwana atajibu,utalia kuomba msaada,
naye atasema: Mimi hapa.
“Kama ukiiondoa nira ya udhalimu,na kunyoosha kidole na kuzungumza maovu,

10nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenuna kutosheleza mahitaji ya walioonewa,ndipo nuru yenu itakapongʼaa gizani,nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.

11Bwana atakuongoza siku zote,atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame,
naye ataitia nguvu mifupa yako.Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri,kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.

12Watu wako watajenga tena magofu ya zamanina kuinua misingi ya kale;utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka,Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.

13“Kama ukitunza miguu yako isivunje Sabato,na kutokufanya kama vile upendavyo katika siku yangu takatifu,kama ukiita Sabato siku ya furahana siku takatifu ya Bwana ya kuheshimiwa,kama utaiheshimu kwa kutoenendakatika njia zako mwenyewe,na kutokufanya yakupendezayoau kusema maneno ya upuzi,

14ndipo utakapojipatia furaha yako katika Bwana,nami nitakufanya upande juu ya miinuko ya nchina kusherehekea urithi wa Yakobo baba yako.”Kinywa cha Bwana kimenena haya.