Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 22 mistari

Yeremia 8

Yeremia • Sura 8 / 52

1“ ‘Wakati huo, asema Bwana, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao.

2Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyotapakaa juu ya ardhi.

3Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.’

Dhambi Na Adhabu

4“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana:“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?Je, mtu anapopotea harudi?

5Kwa nini basi watu hawa walipotea?Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?Wanangʼangʼania udanganyifuna wanakataa kurudi.

6Nimewasikiliza kwa makini,lakini hawataki kusema lililo sawa.Hakuna anayetubia makosa yakeakisema, “Nimefanya nini?”Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewekama farasi anayekwenda vitani.

7Hata korongo aliyeko anganianayajua majira yake yaliyoamriwa,nao njiwa, mbayuwayu na koikoihufuata majira yao ya kurudi.Lakini watu wangu hawajuiBwana anachotaka kwao.

8“ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busarakwa sababu tunayo sheria ya Bwana,”wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishiimeandika kwa udanganyifu?

9Wenye hekima wataaibika,watafadhaika na kunaswa.Kwa kuwa wamelikataa neno la Bwana,hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

10Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,na mashamba yao kwa wamiliki wengine.Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,wote wana tamaa ya kupata zaidi;manabii na makuhani wanafanana,wote wanafanya udanganyifu.

11Wanafunga majeraha ya watu wangubila uangalifu.Wanasema, “Amani, amani,”wakati hakuna amani.

12Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno?Hapana, hawana aibu hata kidogo,
hawajui hata kuona haya.Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,watashushwa chini watakapoadhibiwa,asema Bwana.

13“ ‘Nitayaondoa mavuno yao,asema Bwana.Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu.Hapatakuwepo na tini kwenye mtini,majani yake yatanyauka.Kile nilichowapawatanyangʼanywa.’ ”

14“Kwa nini tunaketi hapa?Kusanyikeni pamoja!Tukimbilie kwenye miji yenye maboma,tukaangamie huko!Kwa kuwa Bwana, Mungu wetuametuhukumu kuangamia,na kutupa maji yenye sumu tunywe,kwa sababu tumemtenda dhambi.

15Tulitegemea amani,lakini hakuna jema lililokuja,tulitegemea wakati wa kupona,lakini kulikuwa hofu tu.

16Mkoromo wa farasi za aduiumesikika kuanzia Dani,kwa mlio wa madume yao ya farasi,nchi yote inatetemeka.Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo,mji na wote waishio ndani yake.”

17“Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali katikati yenu,fira ambao hawawezi kulogwa,
nao watawauma,”asema Bwana.

18Ee Mfariji wangu katika huzuni,moyo wangu umezimia ndani yangu.

19Sikia kilio cha watu wangukutoka nchi ya mbali:“Je, Bwana hayuko Sayuni?Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”
“Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

20“Mavuno yamepita,kiangazi kimekwisha,
nasi hatujaokolewa.”

21Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia;ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.

22Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi?Je, hakuna tabibu huko?Kwa nini basi hakuna uponyajiwa majeraha ya watu wangu?