1Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya majina macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!Ningelia usiku na mchanakwa kuuawa kwa watu wangu.
2Laiti ningekuwa na nyumbaya kukaa wasafiri jangwani,ningewaacha watu wanguna kwenda mbali nao,kwa kuwa wote ni wazinzi,kundi la watu wadanganyifu.
3“Huweka tayari ndimi zao kama upinde,ili kurusha uongo;wamekuwa na nguvu katika nchilakini si katika ukweli.Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,hawanitambui mimi,”asema Bwana.
4“Jihadhari na rafiki zako;usiwaamini ndugu zako.Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,na kila rafiki ni msingiziaji.
5Rafiki humdanganya rafiki,hakuna yeyote asemaye kweli.Wamefundisha ndimi zao kudanganya,wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.
6Unakaa katikati ya udanganyifu;katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”asema Bwana.
7Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:“Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,kwani ni nini kingine niwezacho kufanya
kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?
8Ndimi zao ni mshale wenye sumu,hunena kwa udanganyifu.Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,lakini moyoni mwake humtegea mtego.
9Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”asema Bwana.“Je, nisijilipizie kisasikwa taifa kama hili?”
10Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milimana kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,milio ya ngʼombe haisikiki.Ndege wa angani wametorokana wanyama wamekimbia.
11“Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,makao ya mbweha;nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwaili asiwepo atakayeishi humo.”
12Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na Bwana awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?
13Bwana akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu.
14Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”
15Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu.
16Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”
17Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:“Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,waite wale walio na ustadi kuliko wote.
18Nao waje upesina kutuombolezea,mpaka macho yetu yafurike machozina vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.
19Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!
Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!Ni lazima tuihame nchi yetukwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”
20Basi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana;fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.Wafundisheni binti zenu kuomboleza;fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.
21Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;imewakatilia mbali watoto katika barabarana vijana waume kutoka viwanja vya miji.
22Sema, “Hili ndilo asemalo Bwana:“ ‘Maiti za wanaume zitalalakama mavi katika mashamba,kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,wala hakuna anayekusanya.’ ”
23Hili ndilo asemalo Bwana:“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,
wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,
24lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:kwamba ananifahamu na kunijua mimi,kwamba mimi ndimi Bwana, nitendaye wema,hukumu na haki duniani,
kwa kuwa napendezwa na haya,”asema Bwana.
25“Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema Bwana,
26yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”