1Katika siku za mwishomlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwakama mlima mkuu miongoni mwa milima yote;utainuliwa juu ya vilima,na watu wa mataifa watamiminika humo.
2Mataifa mengi yatakuja na kusema,âNjooni, twendeni mlimani mwa Bwana,kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.Atatufundisha njia zake,ili tuweze kuenenda katika mapito yake.âSheria itatoka Sayuni,neno la Bwana litatoka Yerusalemu.
3Atahukumu kati ya mataifa mengi,na ataamua migogoro ya mataifa
yenye nguvu na yaliyo mbali.Watafua panga zao ziwe majembe,na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,wala hawatajifunza vita tena.
4Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wakena chini ya mtini wake,wala hakuna mtu atakayewaogopesha,kwa kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema.
5Mataifa yote yanaweza kutembeakatika jina la miungu yao;sisi tutatembea katika jina la BwanaMungu wetu milele na milele.
6âKatika siku hiyo,â asema Bwana,ânitawakusanya walemavu;nitawakusanya walio uhamishoni
na wale niliowahuzunisha.
7Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.Bwana atatawala juu yao katika Mlima Sayunikuanzia siku hiyo na hata milele.
8Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi,ee ngome ya Binti Sayuni,milki ya awali itarudishwa kwako,ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.â
9Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:kwani huna mfalme?Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamatekama ya mwanamke
aliye na utungu wa kuzaa?
10Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni,kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,kwa kuwa sasa ni lazima uuache mjiukapige kambi uwanjani.Utakwenda Babeli;huko utaokolewa.Huko Bwana atakukomboakutoka mikononi mwa adui zako.
11Lakini sasa mataifa mengiyamekusanyika dhidi yako.Wanasema, âMwache anajisiwe,macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!â
12Lakini hawayajuimawazo ya Bwana;hawauelewi mpango wake,yeye awakusanyaye kama miganda
kwenye sakafu ya kupuria.
13âInuka upure, ee Binti Sayuni,kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;nitakupa kwato za shabana utavunja vipande vipande mataifa mengi.â
Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Bwana,utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.