1Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi,kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu.Watampiga mtawala wa Israelishavuni kwa fimbo.
2“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi,ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda,kutoka kwako atatokea kwa ajili yanguyeye atakayekuwa mtawala katika Israeli,ambaye asili yake ni kutoka zamani,kutoka milele.”
3Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakatimwanamke aliye na utungu atakapozaana ndugu zake wengine warudikujiunga na Waisraeli.
4Atasimama na kulichunga kundi lakekatika nguvu ya Bwana,
katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake.Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huoukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
5Naye atakuwa amani yao.Ukombozi Na UharibifuWakati Mwashuru atakapovamia nchi yetuna kupita katika ngome zetu,tutawainua wachungaji saba dhidi yake,hata viongozi wanane wa watu.
6Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga,nchi ya Nimrodi kwa upanga.Atatuokoa kutoka kwa Mwashuruatakapoivamia nchi yetu
na kuingia katika mipaka yetu.
7Mabaki ya Yakobo yatakuwakatikati ya mataifa mengikama umande kutoka kwa Bwana,kama manyunyu juu ya majani,ambayo hayamngoji mtuwala kukawia kwa mwanadamu.
8Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa,katikati ya mataifa mengi,kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni,kama mwana simba miongoni
mwa makundi ya kondoo,ambaye anaumiza vibaya na kuwararuakila anapopita katikati yao,
wala hakuna awezaye kuokoa.
9Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako,nao adui zako wote wataangamizwa.
10“Katika siku ile,” asema Bwana,“nitaangamiza farasi zenu katikati yenuna kubomoa magari yenu ya vita.
11Nitaiangamiza miji ya nchi yenuna kuziangusha chini ngome zenu zote.
12Nitaangamiza uchawi wenuna hamtapiga tena ramli.
13Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchongana mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu;hamtasujudia tenakazi ya mikono yenu.
14Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenuna kubomoa miji yenu.
15Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabujuu ya mataifa ambayo hayajanitii.”