1Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia:Huyu mtu alimwambia Ithieli,naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:
2âMimi ni mjinga kuliko wanadamu wote;sina ufahamu wa kibinadamu.
3Sijajifunza hekima,wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.
4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka?Ni nani ameshakusanya upepo
kwenye vitanga vya mikono yake?Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake?Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia?Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani?Niambie kama unajua!
5âKila neno la Mungu ni kamilifu;yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.
6Usiongeze kwenye maneno yake,ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.
7âNinakuomba vitu viwili, Ee Bwana;usininyime kabla sijafa:
8Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo;usinipe umaskini wala utajiri,
bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
9Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukanana kusema, âBwana ni nani?âAu nisije nikawa maskini nikaiba,nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.
10âUsimchongee mtumishi kwa bwana wake,asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo.
11âWako watu wale ambao huwalaani baba zaona wala hawawabariki mama zao;
12wale ambao ni safi machoni pao wenyewekumbe hawakuoshwa uchafu wao;
13wale ambao daima macho yao ni ya kiburi,ambao kutazama kwao ni kwa dharau;
14wale ambao meno yao ni pangana ambao mataya yao yamewekwa visukuwaangamiza maskini katika nchi,na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.
15âMruba anao binti wawili waliao,âNipe! Nipe!â
âKuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe,naam, viko vinne visivyosema, âYatosha!â:
16Ni kaburi, tumbo lisilozaa,nchi isiyoshiba maji kamwe,
na moto, usiosema kamwe, âYatosha!â
17âJicho lile limdhihakilo baba,lile linalodharau kumtii mama,litangĘźolewa na kunguru wa bondeni,litaliwa na tai.
18âKuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana,naam, vinne nisivyovielewa:
19Ni mwendo wa tai katika anga,mwendo wa nyoka juu ya mwamba,mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari,nao mwendo wa mtu pamoja na msichana.
20âHuu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi,hula akapangusa kinywa chake na kusema,
âSikufanya chochote kibaya.â
21âKwa mambo matatu nchi hutetemeka,naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:
22Mtumwa awapo mfalme,mpumbavu ashibapo chakula,
23mwanamke asiyependwa aolewapo,naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.
24âVitu vinne duniani vilivyo vidogo,lakini vina akili nyingi sana:
25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo,hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.
26Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogohata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.
27Nzige hawana mfalme,hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.
28Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono,hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.
29âViko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao,naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha:
30simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama,asiyerudi nyuma kwa chochote;
31jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu,naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka.
32âIkiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe,au kama umepanga mabaya,
basi funika mdomo wako na mkono wako.
33Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi,na pia kule kufinya pua hutoa damu,
kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.â