Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 5 mistari

Zaburi 127

Zaburi • Sura 127 / 150

Bila Mungu, Kazi Ya Mwanadamu Haifai
Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni.

1Bwana asipoijenga nyumba,wajengao hufanya kazi bure.Bwana asipoulinda mji,walinzi wakesha bure.

2Mnajisumbua bure kuamka mapemana kuchelewa kulala,mkitaabikia chakula:kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.

3Wana ni urithi utokao kwa Bwana,watoto ni zawadi kutoka kwake.

4Kama mishale mikononi mwa shujaandivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.

5Heri mtu ambaye podo lakelimejazwa nao.Hawataaibishwa wanaposhindanana adui zao langoni.