Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 6 mistari

Zaburi 128

Zaburi • Sura 128 / 150

Thawabu Ya Kumtii Bwana
Wimbo wa kwenda juu.

1Heri ni wale wote wamchao Bwana,waendao katika njia zake.

2Utakula matunda ya kazi yako;baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaaondani ya nyumba yako;wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeitunikuizunguka meza yako.

4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwamtu amchaye Bwana.

5Bwana na akubariki kutoka Sayunisiku zote za maisha yako,na uone mafanikio ya Yerusalemu,

6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.