Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 3 mistari

Zaburi 131

Zaburi • Sura 131 / 150

Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana,macho yangu hayajivuni;sijishughulishi na mambo makuu kunizidiwala mambo ya ajabu mno kwangu.

2Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu;kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake,kama mtoto aliyeachishwa kunyonyandivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.

3Ee Israeli, mtumaini Bwanatangu sasa na hata milele.