1Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.
2Ee Bwana, sikia sauti yangu.Masikio yako na yawe masikivukwa kilio changu unihurumie.
3Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi,Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?
4Lakini kwako kuna msamaha,kwa hiyo wewe unaogopwa.
5Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea,katika neno lake naweka tumaini langu.
6Nafsi yangu inamngojea Bwanakuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,naam, kuliko walinziwaingojeavyo asubuhi.
7Ee Israeli, mtumaini Bwana,maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma,
na kwake kuna ukombozi kamili.
8Yeye mwenyewe ataikomboa Israelikutoka dhambi zao zote.