Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 7 mistari

Zaburi 14

Zaburi • Sura 14 / 150

Uovu Wa Wanadamu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Mpumbavu anasema moyoni mwake,“Hakuna Mungu.”Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa;hakuna hata mmoja atendaye mema.

2Bwana anawachungulia wanadamu chinikutoka mbinguniaone kama wako wenye akili,wowote wanaomtafuta Mungu.

3Wote wamepotoka,wameharibika wote pamoja,hakuna atendaye mema.Naam, hakuna hata mmoja!

4Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:wale ambao huwala watu wangukama watu walavyo mkate,hao ambao hawamwiti Bwana?

5Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu,maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.

6Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini,bali Bwana ndiye kimbilio lao.

7Laiti wokovu wa Israeliungalikuja kutoka Sayuni!Wakati Bwana arejeshapowafungwa wa watu wake,Yakobo na ashangilie,Israeli na afurahi!