Kitu Mungu Anachotaka
Zaburi ya Daudi.
1Bwana, ni nani awezaye kukaakatika Hekalu lako?Nani awezaye kuishikatika mlima wako mtakatifu?
2Ni yule aendaye pasipo mawaa,atendaye yaliyo haki,asemaye kweli toka moyoni mwake,
3na hana masingizio ulimini mwake,asiyemtenda jirani yake vibaya,na asiyemsingizia mwenzake,
4ambaye humdharau mtu mbaya,lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana,yule atunzaye kiapo chakehata kama anaumia.
5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.
Mtu afanyaye hayakamwe hatatikisika.