Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 11 mistari

Zaburi 16

Zaburi • Sura 16 / 150

Sala Ya Matumaini
Utenzi wa Daudi.

1Ee Mungu, uniweke salama,kwa maana kwako nimekimbilia.

2Nilimwambia Bwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu;pasipo wewe sina jambo jema.”

3Kwa habari ya watakatifu walioko duniani,ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.

4Huzuni itaongezeka kwa walewanaokimbilia miungu mingine.Sitazimimina sadaka zao za damuau kutaja majina yao midomoni mwangu.

5Bwana umeniwekea fungu langu na kikombe changu;umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.

6Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,hakika nimepata urithi mzuri.

7Nitamsifu Bwana ambaye hunishauri,hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.

8Nimemweka Bwana mbele yangu daima.Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.

9Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;mwili wangu nao utapumzika salama,

10kwa maana hutaniacha kaburini,wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.

11Umenijulisha njia ya uzima;utanijaza na furaha mbele zako,pamoja na furaha za milelekatika mkono wako wa kuume.