Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 9 mistari

Zaburi 28

Zaburi • Sura 28 / 150

Kuomba Msaada
Zaburi ya Daudi.

1Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu;usiwe kwangu kama kiziwi.Kwa sababu ukinyamazanitafanana na walioshuka shimoni.

2Sikia kilio changu unihurumieninapokuita kwa ajili ya msaada,niinuapo mikono yangu kuelekeaPatakatifu pa Patakatifu pako.

3Usiniburute pamoja na waovu,pamoja na hao watendao mabaya,ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri,lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

4Walipe sawasawa na matendo yao,sawasawa na matendo yao maovu;walipe sawasawa na kazi za mikono yao,uwalipe wanavyostahili.

5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana,na yale ambayo mikono yake imetenda,atawabomoa na kamwehatawajenga tena.

6Bwana asifiwe,kwa maana amesikia kilio changu
nikimwomba anihurumie.

7Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.Moyo wangu unarukaruka kwa furahanami nitamshukuru kwa wimbo.

8Bwana ni nguvu ya watu wake,ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

9Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;uwe mchungaji wao na uwabebe milele.