1Mpeni Bwana, enyi mashujaa,mpeni Bwana utukufu na nguvu.
2Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
3Sauti ya Bwana iko juu ya maji;Mungu wa utukufu hupiga radi,
Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
4Sauti ya Bwana ina nguvu;sauti ya Bwana ni tukufu.
5Sauti ya Bwana huvunja mierezi;Bwana huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.
6Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,Sirioni*urukaruke kama mwana nyati.
7Sauti ya Bwana hupiga kwa mialiya umeme wa radi.
8Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Bwana huzalisha ayala,na huuacha msitu wazi.Hekaluni mwake wote wasema,“Utukufu!”
10Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
11Bwana huwapa watu wake nguvu;Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.
Tanbihi
Yaani Mlima Hermoni.