Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 12 mistari

Zaburi 30

Zaburi • Sura 30 / 150

Maombi Ya Shukrani
Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

1Nitakutukuza wewe, Ee Bwana,kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,na hukuacha adui zanguwashangilie juu yangu.

2Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidiena wewe umeniponya.

3Ee Bwana, umenitoa Kuzimu,umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

4Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake;lisifuni jina lake takatifu.

5Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,bali upendo wake hudumu siku zote.Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,lakini asubuhi kukawa na furaha.

6Nilipofanikiwa nilisema,“Sitatikiswa kamwe.”

7Ee Bwana, uliponijalia,uliuimarisha mlima wangu,lakini ulipouficha uso wakonilifadhaika.

8Kwako wewe, Ee Bwana, niliita,kwa Bwana niliomba rehema:

9“Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?Katika kushuka kwangu shimoni?Je, mavumbi yatakusifu?Je, yatatangaza uaminifu wako?

10Ee Bwana, unisikie na kunihurumia,Ee Bwana, uwe msaada wangu.”

11Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

12ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.