1Nilisema, āNitaziangalia njia zanguna kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;nitaweka lijamu kinywani mwanguwakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.ā
2Lakini niliponyamaza kimya na kutulia,hata pasipo kusema lolote jema,
uchungu wangu uliongezeka.
3Moyo wangu ulipata moto ndani yangu,nilipotafakari, moto uliwaka,
ndipo nikasema kwa ulimi wangu:
4āEe Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yanguna hesabu ya siku zangu;nijalie kujua jinsi maisha yanguyanavyopita upesi.
5Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;muda wangu wa kuishi ni kama
hauna thamani kwako.Maisha ya kila mwanadamuni kama pumzi.
6Hakika kila binadamu ni kama njoziaendapo huku na huko:hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili;anakusanya mali nyingi,
wala hajui ni nani atakayeifaidi.
7āLakini sasa Bwana, nitafute nini?Tumaini langu ni kwako.
8Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote,usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.
9Nilinyamaza kimya,sikufumbua kinywa changu,
kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.
10Niondolee mjeledi wako,nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako.
11Unakemea na kuadhibu wanadamukwa ajili ya dhambi zao;unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo:kila mwanadamu ni kama pumzi tu.
12āEe Bwana, usikie maombi yangu,usikie kilio changu unisaidie,
usiwe kiziwi kwa kulia kwangu.Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni,kama walivyokuwa baba zangu wote,
13Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tenakabla sijaondoka na nisiwepo tena.ā