1Nilimngoja Bwana kwa saburi,naye akaniinamia, akasikia kilio changu.
2Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,kutoka matope na utelezi;akaiweka miguu yangu juu ya mwambana kunipa mahali imara pa kusimama.
3Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.Wengi wataona na kuogopana kuweka tumaini lao kwa Bwana.
4Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
5Ee Bwana Mungu wangu,umefanya mambo mengi ya ajabu.Mambo uliyopanga kwa ajili yetuhakuna awezaye kukuhesabia;kama ningesema na kuyaelezea,yangekuwa mengi mno kuyaelezea.
6Dhabihu na sadaka hukuvitaka,lakini umefungua masikio yangu;*sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambihukuzihitaji.
7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:imeandikwa kunihusu katika kitabu.
8Ee Mungu wangu,natamani kuyafanya mapenzi yako;
sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”
9Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,sikufunga mdomo wangu,
Ee Bwana, kama ujuavyo.
10Sikuficha haki yako moyoni mwangu;ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.Sikuficha upendo wako na kweli yakombele ya kusanyiko kubwa.
11Ee Bwana, usizuilie huruma zako,upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
12Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,nao moyo unazimia ndani yangu.
13Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,waaibishwe na kufadhaishwa;wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,warudishwe nyuma kwa aibu.
15Wale waniambiao, “Aha! Aha!”wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16Lakini wote wakutafutaowashangilie na kukufurahia,wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,“Bwana atukuzwe!”
17Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;Bwana na anifikirie.Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;Ee Mungu wangu, usikawie.
Tanbihi
Au: bali mwili uliniandalia.