1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewanayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.
3Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka,milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake.
4Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu,mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi.
5Mungu yuko katikati yake, hautaanguka,Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka,Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka.
7Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi,Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8Njooni mkaone kazi za Bwanajinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9Anakomesha vita hata miisho ya dunia,anakata upinde na kuvunjavunja mkuki,
anateketeza ngao kwa moto.
10“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu;nitatukuzwa katikati ya mataifa,
nitatukuzwa katika dunia.”
11Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi;Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.