Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 9 mistari

Zaburi 47

Zaburi • Sura 47 / 150

Mtawala Mwenye Enzi Yote
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.

1Pigeni makofi, enyi mataifa yote,mpigieni Mungu kelele za shangwe!

2Jinsi gani alivyo wa kutisha, Bwana Aliye Juu Sana,Mfalme mkuu juu ya dunia yote!

3Ametiisha mataifa chini yetuwatu wengi chini ya miguu yetu.

4Alituchagulia urithi wetu,fahari ya Yakobo, aliyempenda.

5Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,Bwana kwa sauti za tarumbeta.

6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa,mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa.

7Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote,mwimbieni zaburi za sifa.

8Mungu anatawala juu ya mataifa,Mungu ameketi juu ya kiti chake cha enzi kitakatifu.

9Wakuu wa mataifa wanakusanyikakama watu wa Mungu wa Abrahamu,kwa kuwa wafalme wa dunia ni mali ya Mungu;yeye ametukuka sana.