1Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,katika mji wa Mungu wetu,
mlima wake mtakatifu.
2Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana,furaha ya dunia yote.Kama vilele vya juu sana vya Safoni*ni Mlima Sayuni,mji wa Mfalme Mkuu.
3Mungu yuko katika ngome zake;amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.
4Wakati wafalme walipounganisha nguvu,waliposonga mbele pamoja,
5walimwona nao wakashangaa,wakakimbia kwa hofu.
6Kutetemeka kuliwashika huko,maumivu kama ya mwanamke
mwenye utungu wa kuzaa.
7Uliwaangamiza kama meli za Tarshishizilizovunjwa na upepo wa mashariki.
8Kama tulivyokuwa tumesikia,ndivyo tulivyoonakatika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,katika mji wa Mungu wetu:
Mungu ataufanya uwe salama milele.
9Ee Mungu, hekaluni mwakotunatafakari upendo wako usiokoma.
10Ee Mungu, kama jina lako lilivyo,sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,
mkono wako wa kuume umejazwa na haki.
11Mlima Sayuni unashangilia,vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako.
12Tembeeni katika Sayuni,uzungukeni mji,
hesabuni minara yake;
13yatafakarini vyema maboma yake,angalieni ngome zake,ili mpate kusimulia habari zakekwa kizazi kijacho.
14Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele;atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.
Tanbihi
Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini.