1Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni;kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa.
2Ewe usikiaye maombi,kwako wewe watu wote watakuja.
3Tulipokuwa tumefunikwa kabisa na dhambi,wewe ulisamehe makosa yetu.
4Heri wale uliowachaguana kuwaleta karibu ili waishi katika nyua zako!Tunashibishwa kwa mema ya nyumba yako,mema ya Hekalu lako takatifu.
5Unatujibu kwa matendo ya kushangaza ya haki,Ee Mungu Mwokozi wetu,tumaini la miisho yote ya dunianina la bahari zilizo mbali sana,
6uliyeumba milima kwa uwezo wako,ukiwa umejivika nguvu,
7uliyenyamazisha dhoruba za bahari,ngurumo za mawimbi yake,
na ghasia za mataifa.
8Wale wanaoishi mbali sanawanaogopa maajabu yako,kule asubuhi ipambazukiapona kule jioni inakofifilia
umeziita nyimbo za furaha.
9Waitunza nchi na kuinyeshea,waitajirisha kwa wingi.Vijito vya Mungu vimejaa majiili kuwapa watu nafaka,
kwa maana wewe umeviamuru.
10Umeilowesha mifereji yakena kusawazisha kingo zake;umeilainisha kwa manyunyuna kuibariki mimea yake.
11Umeuvika mwaka taji ya baraka,magari yako yanafurika kwa wingi.
12Mbuga za majani za jangwani umezineemesha;vilima vimevikwa furaha.
13Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama,na mabonde yamepambwa kwa mavuno;
vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.