1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!
2Imbeni utukufu wa jina lake;
mpeni sifa zake kwa utukufu!
3Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako!Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba
adui wananyenyekea mbele zako.
4Dunia yote yakusujudia,wanakuimbia wewe sifa,
wanaliimbia sifa jina lako.”
5Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda,mambo ya kutisha aliyoyatenda
miongoni mwa wanadamu!
6Alifanya bahari kuwa nchi kavu,wakapita kati ya maji kwa miguu,
njooni, tumshangilie.
7Yeye hutawala kwa uwezo wake milele,macho yake huangalia mataifa yote:
waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake.
8Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu,sauti ya sifa yake isikike,
9ameyahifadhi maisha yetuna kuizuia miguu yetu kuteleza.
10Ee Mungu, wewe ulitujaribu,ukatusafisha kama fedha.
11Umetuingiza kwenye nyavuna umetubebesha mizigo mizito
migongoni mwetu.
12Uliwaruhusu watu watukalie vichwani,tulipita kwenye moto na kwenye maji,lakini ulituleta kwenye nchiiliyojaa utajiri tele.
13Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwana kukutimizia nadhiri zangu:
14nadhiri ambazo midomo yangu iliahidina nilizotamka kwa kinywa changu
nilipokuwa katika shida.
15Nitakutolea dhabihu za wanyama wanonona sadaka za kondoo dume,
nitakutolea mafahali na mbuzi.
16Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu,nami niwaambie aliyonitendea.
17Nilimlilia kwa kinywa changu,sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu.
18Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu,Bwana asingekuwa amenisikiliza;
19lakini hakika Mungu amenisikilizana amesikia sauti yangu katika maombi.
20Sifa apewe Mungu,ambaye hakulikataa ombi langu
wala kunizuilia upendo wake!