1Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,wamelinajisi Hekalu lako takatifu,
wameifanya Yerusalemu kuwa magofu.
2Wametoa maiti za watumishikuwa chakula cha ndege wa anganina nyama ya watakatifu wakokwa wanyama wa nchi.
3Wamemwaga damu kama majikuzunguka Yerusalemu yote,
wala hakuna yeyote wa kuwazika.
4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka.
5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele?Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?
6Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali,juu ya falme za hao wasioliitia jina lako,
7kwa maana wamemrarua Yakobona kuharibu nchi ya makao yake.
8Usituhesabie dhambi za baba zetu,huruma yako na itujie hima,
kwa maana tu wahitaji mno.
9Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,kwa ajili ya utukufu wa jina lako;tuokoe na kutusamehe dhambi zetukwa ajili ya jina lako.
10Kwa nini mataifa waseme,“Yuko wapi Mungu wenu?”Mbele ya macho yetu,dhihirisha kati ya mataifakwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwaya watumishi wako.
11Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako;kwa nguvu za mkono wako
hifadhi wale waliohukumiwa kufa.
12Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwaoaibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana.
13Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,tutakusifu milele;toka kizazi hadi kizazitutasimulia sifa zako.