Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 5 mistari

Zaburi 93

Zaburi • Sura 93 / 150

Mungu Mfalme

1Bwana anatawala, amejivika utukufu;Bwana amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.Dunia imewekwa imara,haitaondoshwa.

2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;wewe umekuwako tangu milele.

3Bahari zimeinua, Ee Bwana,bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.

4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

5Ee Bwana, sheria zako ni imara;utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.