Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 15 mistari

Zaburi 92

Zaburi • Sura 92 / 150

Wimbo Wa Kumsifu Mungu
Zaburi. Wimbo wa siku ya Sabato.

1Ni vyema kumshukuru Bwanana kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

2kuutangaza upendo wako asubuhi,na uaminifu wako wakati wa usiku,

3kwa zeze yenye nyuzi kumina kwa sauti ya kinubi.

4Ee Bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha,nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako.

5Ee Bwana, tazama jinsi yalivyo makuu matendo yako,tazama jinsi yalivyo ya kina mawazo yako!

6Mjinga hafahamu,mpumbavu haelewi,

7ingawa waovu huchipua kama majanina wote watendao mabaya wanastawi,
wataangamizwa milele.

8Bali wewe, Ee Bwana,utatukuzwa milele.

9Ee Bwana, hakika adui zako,hakika adui zako wataangamia.
Wote watendao mabaya watatawanyika.

10Umeitukuza pembe*yangu kama ile ya nyati dume,mafuta mazuri yamemiminwa juu yangu.

11Macho yangu yamewaona adui zangu wakishindwa,masikio yangu yamesikia maangamizi ya adui zangu waovu.

12Wenye haki watastawi kama mtende,watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

13waliopandwa katika nyumba ya Bwana,watastawi katika nyua za Mungu wetu.

14Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

15wakitangaza, “Bwana ni mkamilifu;yeye ni Mwamba wangu,
na ndani yake hamna uovu.”

Tanbihi

*

Pembe inawakilisha nguvu.