1Usiku kucha kwenye kitanda changunilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;
nilimtafuta, lakini sikumpata.
2Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,katika barabara zake na viwanja;nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.
3Walinzi walinikutawalipokuwa wakizunguka mji.Nikawauliza, “Je, mmemwonayule moyo wangu umpendaye?”
4Kitambo kidogo tu baada ya kuwapitanilimpata yule moyo wangu umpendaye.Nilimshika na sikumwachia aendempaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,
katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.
5Binti za Yerusalemu, ninawaagizakwa paa na kwa ayala wa shambani:Msichochee wala kuamsha mapenzihata yatakapotaka yenyewe.
6Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwanikama nguzo ya moshi,anayenukia manemane na uvumbailiyotengenezwa kwa vikolezo vyote
vya mfanyabiashara?
7Tazama! Ni gari la Solomonilisindikizwalo na mashujaa sitini,
walio wakuu sana wa Israeli,
8wote wamevaa panga,wote wazoefu katika vita,kila mmoja na upanga wake pajani,wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.
9Mfalme Solomoni alijitengenezea gari;alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.
10Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha,kitako chake kwa dhahabu.Kiti chake kilipambwa kwa zambarau,gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo
na binti za Yerusalemu.
11Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni,mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji,taji ambalo mama yake alimvikasiku ya arusi yake,
siku ambayo moyo wake ulishangilia.